ZLATAN IBRAHIMOVICH: SIMJUI PEP GUARDIOLA
![]() |
| Guardiola sasa ni kocha wa Man City |
Zlatan amesema kuwa anaamini yeye na kocha wake, Jose Mourinho wanaelewana falsafa kwa kuwa ni watu wa ushindi lakini alipoulizwa kuhusu Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alisema: “Nilikuwa namjua Guardiola wa Barcelona lakini huyu wa sasa simjui.”
Katika mahojiano hayo ambayo yamerushwa hewani leo Ijumaa, Zlatana amesema kuwa Guardiola ni kocha mzuri na alichokuwa akikijua kipindi cha nyuma kuhusu kocha huyo hawezi kusema ndivyo alivyo sasa.
“Kwa sasa simjui, kipindi kile kila mtu alijua ni kocha mzuri na nsiyo maana alifanikiwa, anafanyaje kazi leo, mimi sijui, anaendeleaje hilo nalo sijui kwa kuwa siyo kocha wangu,” alisema Zlatan.



No comments:
Post a Comment