Wednesday, 19 October 2016

TAZAMA JINSI GUADIOLA ALIVYO KARIBISHWA ENGLAND


VIDEO JINSI CHELSEA ILIVYO IADHIBU LEISTER CITY KWENYE EPL


ANGALIA GOLI LA KICHUYA DHIDI YA YANGA


Tennis: Kyrgios afungiwa kucheza wiki nane

Na Salama Ngale

Muaustralia Nick Kyrgios amefungiwa kwa wiki nane na kutozwa faini ya dola za kimarekani 25,000 kwa utovu wa nidhamu-ikiwa ni pamoja na kucheza ovyo wiki iliyopita michuano ya Shaghai Masters.

Nick mwenye miaka 21 amekuwa akigongesha mpira juu ya wavu mara kadhaa katika mchezo aliofungwa Mischa Zverev kwa seti 6-3 6-1 .
Mchezaji huyo nambari 14 kwa ubora duniani ameomba radhi kwa tukio hilo na kusema atafanyia kazi wakati huu akiwa kifungoni.
Wiki iliyopita Muingereza Andy Murray alisema hafikirii kuwa faini pekee itakuwa adhabu tosha.
Mwaka 2015 Kyrgios alifungiwa siku 28 na faini ya dola 25,000 baada ya kutoa maneno ya kashfa kwa mpenzi wa Stan Wawrinka katika michuano ya kombe la Rogers.

TAKWIMU ZAMBEBA KIPA SIMBA, ASHIKILIA USUKANI WA KIPA BORA


VICENT
Na salama Ngale 
Kipa wa Simba, Vincent Angban mpaka sasa ndiye aliyecheza mechi nyingi bila kuruhusu bao ‘clean sheet’, akifanya hivyo kwenye michezo sita kati ya tisa iliyocheza Simba huku akisimama golini mechi zote, sawa na dakika 810.

Muivory Coast huyo aliyetoswa na Azam majaribioni mwanzoni mwa msimu kwa kile walichosema kiwango chake ni hafifu, mpaka sasa amefanikiwa kuiweka Simba kileleni mwa msimamo, huku akiwa ameruhusu mabao matatu tu katika mechi tatu pekee.

Simba inaungana na Yanga ambayo pia imeruhusu idadi hiyo ya mabao, ikiwa ni idadi ndogo zaidi, lakini tofauti ni kwamba lango la Yanga limelindwa na Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’kwa nyakati tofauti.

Akizungumzia clean sheet, Angban alisema ni jambo la furaha kwake na shukrani kwa wachezaji wenzake pamoja na uwezo binafsi anayopigana kuhakikisha anauonyesha awapo uwanjani.

“Ni jambo zuri, lakini siku zote haya ndiyo matokeo ya mtu binafsi na timu kwa ujumla. Siwezi kusema kuhusu ni clean sheet ngapi nifikishe kwa sababu ninacheza kwa kujituma kwa ajili ya timu yangu ili iendelee kufanya vizuri,” alisema kipa huyo.

Mechi Simba ilizoruhusu bao ni katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, ushindi wa 3-1 dhidi ya Ndanda na sare ya 1-1 na Yanga, huku ikizikazia Kagera Sugar (2-0), Mtibwa Sugar (2-0), Majimaji (4-0), JKT Ruvu (0-0), Azam (1-0) na Mbeya City (2-0).

Wednesday, 12 October 2016

POGBA APIGA BAO LA MWENDO KASI UFARANSA IKIILAZA UHOLANZI BAO 1-0


Holland (4-3-3): Stekelenburg, Karsdorp, Bruma, van Dijk, Blind, Strootman, Wijnaldum (Dost 61), Promes (Depay 16), Morishige (Willems 83), Klaassen, Janssen.
Subs not used: Zoet, Veltman, de Vrij, Kongolo, Clasie, Toornstra, Vilhena, De Jong, Vorm
Booked: Strootman, Morishige  
France (4-2-3-1): Lloris, Sidibe, Varane, Koscielny, Kurzawa, Pogba, Matuidi, Sissoko, Griezmann (Kante 90), Payet (Martial 66), Gameiro (Gignac 79).
Subs not used: Mandanda, Laporte, Fekir, Kimpembe, Cabaye, Digne, Corchia, Coman, Areola.
Goal: Pogba 30

Booked: Pogba

HUYU TYSON FURY KIBOKO, KILA SIKU ANAIBUKA NA KITUKO KIPYA



Kati ya bondia anayeongoza kwa vituko kwa sasa ni Tyson Fury Wa Uingereza.
Mara atangaze kuwa

Argentina watandikwa Peru mechi ya kufuzu Kombe la Dunia



Mechi za Raundi ya 10 ya nchi za kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa Shirikisho lao CONMEBOL kusaka nchi 4 zitakazotinga moja kwa moja huko Urusi Mwaka 2018 kwenye Fainali

Serge Aurier aokoa maisha ya mchezaji wa Mali


Beki wa klabu ya Paris Saint-Germain kutoka Ivory Coast Serge Aurier amesifiwa sana baada ya

Liverpool v Man Utd: Uteuzi wa refa Anthony Taylor wakosolewa



Image caption Mwamuzi Anthony Taylor alizaliwa Wythenshawe, maili 10kutoka uwanja wa Manchester United

Mkuu wa zamani wa marefa Uingereza Keith Hackett amekosoa uteuzi wa refa kutoka Manchester Anthony Taylor kuwa mwamuzi wa mechi ya Ligi ya Premia kati ya Liverpool na Manchester United.
Taylor huishi maili sita kutoka Old Trafford, na Hackett anaamini huenda hilo likasababisha madai wa kupendelea upande mmoja.
"Hakuna anayetilia sana uadilifu wake," Hackett alisema.
"Lakini je, kitu kikienda mrama? Itakuwa vigumu kwa baadhi kuvumilia."
Taylor hana uhusiano wowote na United lakini hushabikia klabu ya Ligi ya Taifa ya Kaskazini ya Altrincham.
Hackett anasema inashangaza ikizingatiwa kwamba Mark Clattenburg angepatikana siku hiyo ya Jumatatu.
Badala yake Clattenburg, ambaye ni shabiki wa Newcastle United, ataudumu kama mwamuzi wa nne mechi nyingine wikendi.
Tayari mashabiki wa Liverpool wameanza kulalamika mitandao ya kijamii kuhusu uteuzi wa Taylor.