Beki wa kushoto anayechea katika Ligi Kuu
ya England 'Premier League' akiwa ni mchezaji wa timu ya Crystal
Palace, Pape Souare amejeruhiwa katika ajali mbaya ya gari alipokuwa
katika mitaa ya Jiji la Londo, ambapo ksa sasa yupo hospitali akipata
Straika
mkongwe wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amefunguka mengi
katika mahojiano marefu ya kwanza aliyoyafanya na kituo cha runinga na
MUTV huku akigusia mchezo wa Manchester Derby dhidi ya Manchester City.
Guardiola sasa ni kocha wa Man City
Zlatan
amesema kuwa anaamini yeye na kocha wake, Jose Mourinho wanaelewana
falsafa kwa kuwa ni watu wa ushindi lakini alipoulizwa kuhusu Kocha wa
Manchester City, Pep Guardiola alisema: “Nilikuwa namjua Guardiola wa
Barcelona lakini huyu wa sasa simjui.”
Katika mahojiano hayo
ambayo yamerushwa hewani leo Ijumaa, Zlatana amesema kuwa Guardiola ni
kocha mzuri na alichokuwa akikijua kipindi cha nyuma kuhusu kocha huyo
hawezi kusema ndivyo alivyo sasa.
“Kwa sasa simjui, kipindi kile
kila mtu alijua ni kocha mzuri na nsiyo maana alifanikiwa, anafanyaje
kazi leo, mimi sijui, anaendeleaje hilo nalo sijui kwa kuwa siyo kocha
wangu,” alisema Zlatan.
TEMEKE YAANZA NA MOTO AIRTEL RISING STARS
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM PAZIA
la michuano Taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel
Rising Stars jana lilifunguliwa katika uwanja wa Kukumbukumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam ambapo timu ya wavulana ya Temeke ilitoa onyo kali
kwa timu shiriki kwa kuifunga Kinondoni 4-1. Mchezo
huo ulitanguliwa na mechi ya wasichana kati ya Arusha na Lindi ambapo
Arusha waliibuka na ushindi wa 2-0. Magoli ya Arusha yalifungwa na Eva
Michael dakika ya 39 kwa njia ya penalti na pili likifungwa na Warda
Alfonce dakika ya 60.
Mchezaji
wa Arusha, Diana Mosses (kulia) akiwania mpira na beki wa Lindi , Neema
Hashim katika mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja
wa Karume jijini Dar es Salaam jana Katika
mchezo wa Temeke na Kinondoni, Temeke walianza kwa kasi ya aina yake na
kupeleka mashambuliazi ya mara kwa mara langoni mwa Kinondoni huku
Kinondoni wakionekana kuzidiwa katika kila idara. Temeke
waliandika bao la kwanza kupitia kwa Ramadhan Kawambwa kaika dakika ya
14, kwa njia ya penati baada ya mchezaji wa Temeke kufanyiwa madhambi
katika eneo la hatari. Goli hilo lilipokelewa kwa shangwa na mashabiki
wa Temeke. Temeke
awalipata bao lao la pili kupitia kwa Abirahi Uihuro mnamo dakika ya 34
ambaye aligongeana mpira kwa uzuri na Ismail Kovu na kisha kumchambua
kipa wa Kinondoni kwa umaridadi wa hali ya juu na kuukwamisha mpira huo
kimiani. Mohammed
Mbegu aliifungia Temeke bao la tatu katika dakika ya 40 na kuzidi
kuzamisha jahazi la Kinondoni ambao walinekana kama vile wamesimama
wakati mchezo ukiendelea. Rosea
Mpoma aliwaliza kwa mara nyingine tena Arusha baada ya kuifungia Temeke
bao la tano katika dakika ya 53 baada ya kuachia shuti kali na kuzama
moja kwa moja wavuni. Alikuwa
ni Abirahi Uihuro tena, ambaye aliiandikia Temeka bao la nne mnamo
dakika ya 28 ya kipindi cha pili baada ya kuunganisha krosi iliyochongwa
na Mohammed Mbegu kutoka upande wa kushoto mwa uwanja na kuendeleza
karamu ya magoli kwa Temeke. Kinondoni
walipata goli ya kufuta machozi mnamo dakika 36, likifungwa na Shaban
Mangula baada ya mabeki ya Temeke kushindwa kuokoa mpira wa kona. Michuano
hiyo ya Airtel Rising Stars itaendelea kesho kwenye uwanja wa Karume
jijini Dar es Salaam na kufikia tamati Jumapili, Septemba 11.