![]() |
| VICENT |
Na salama Ngale
Kipa
wa Simba, Vincent Angban mpaka sasa ndiye aliyecheza mechi nyingi bila
kuruhusu bao ‘clean sheet’, akifanya hivyo kwenye michezo sita kati ya
tisa iliyocheza Simba huku akisimama golini mechi zote, sawa na dakika
810.
Muivory
Coast huyo aliyetoswa na Azam majaribioni mwanzoni mwa msimu kwa kile
walichosema kiwango chake ni hafifu, mpaka sasa amefanikiwa kuiweka
Simba kileleni mwa msimamo, huku akiwa ameruhusu mabao matatu tu katika
mechi tatu pekee.
Simba
inaungana na Yanga ambayo pia imeruhusu idadi hiyo ya mabao, ikiwa ni
idadi ndogo zaidi, lakini tofauti ni kwamba lango la Yanga limelindwa na
Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’kwa nyakati tofauti.
Akizungumzia
clean sheet, Angban alisema ni jambo la furaha kwake na shukrani kwa
wachezaji wenzake pamoja na uwezo binafsi anayopigana kuhakikisha
anauonyesha awapo uwanjani.
“Ni
jambo zuri, lakini siku zote haya ndiyo matokeo ya mtu binafsi na timu
kwa ujumla. Siwezi kusema kuhusu ni clean sheet ngapi nifikishe kwa
sababu ninacheza kwa kujituma kwa ajili ya timu yangu ili iendelee
kufanya vizuri,” alisema kipa huyo.

No comments:
Post a Comment